Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wydad yaitumia salam Simba

Wydad Final Wydad yaitumia salam Simba

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wapinzani wa Simba Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), timu ya Wydad Casablanca jana Desemba 6 imecheza mechi ya Ligi Kuu Morocco na kushinda mabao 3-1 ikiifunga Mouloudia Club of Oujda.

Wydad itacheza dhidi ya Simba Desemba 9 jijini Marrakech katika mechi ya tatu hatua ya makundi CAFCL na kwa matokeo waliyopata leo yataamsha morali ikiwa ni timu pekee katika kundi B ambayo haina pointi hadi sasa wakifungwa mechi mbili za awali.

Simba ilicheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Novemba 9 dhidi ya Namungo na kutoka sare ya bao 1-1 na baada ya hapo imecheza mechi mbili za CAFCL dhidi ya ASEC Mimosas na Jwaneng Galaxy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live