Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wydad yainyuka Al Ahly na kutwaa Ubingwa wa Afrika

Wydad Casablanka Wydad wakisherehekea ushindi

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabao ya dakika ya 15 na 48 yakifungwa na Zouhair El Moutaraji yameipa Wydad AC ya Morocco ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wababe wa Misri, Al Ahly.

Al Ahly ambao walikuwa wakitetea taji hilo, licha ya kushambulia muda mwingi katika mchezo huo wa Mei 30, 2022 wameshindwa kufurukuta katika fainali kwenye Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca, Morocco.

Ubingwa huo ambao ni wa tatu kwa Wydad unawapa Dola 2,500,000 (Tsh bilioni 5.7) wakati Al Ahly wameambulia Dola 1,250,000 (Tsh bilioni 2.7) kwa kushika nafasi ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live