Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wydad wamecheza jana, Simba imesogezwa mbele - Mchambuzi

Simba Botswana Yy Wydad wamecheza jana, Simba imesogezwa mbele - Mchambuzi

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Master Tindwa amesema kuwa licha ya Timu ya Wydad Casablanca kucheza mchezo wake wa Ligi nchini Mirsi jana, bado itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Simba SC, Jumamosi ijayo nchini humo.

Tindwa amesema hayo kupitia HiliGame ya Clouds FM leo asubuhi huku akishangazwa na Timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya kimataifa, kubadilishiwa ratiba ya Ligi na mechi zao kusogezwa mbele.

“Jana Wydad wamecheza mechi yao ya Ligi, na ikumbukwe mechi zao tano (5) za mwisho zote wamepoteza tatu ni za ligi (3) na mbili (2) za CAFCL. Lakini jana wameshinda 3-1 kwa mara ya kwanza “

“Wydad wamecheza jana na wanacheza tena Jumamosi dhidi ya Simba CAFCL, Mamelodi pia wamecheza jana lakini sisi huku timu zinaomba zisogezewe mbele mechi zao,” amesema Master Tindwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live