Wapinzani wa Simba SC kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Wydad Casablanca wanatarajia kuingia nchini kesho Aprili 19, 2023 majira ya saa tano asubuhi.
Akizungumza na wanahabari mapema hii leo, Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema, maandalizi ya mchezo huo yameanza rasmi na hivyo kuwaomba mashabiki kufika kwa wingi uwanjani ili kuweza kuibuka na ushindi katika mechi hiyo ya robo fainali itakayopigwa Jumamosi Aprili 22, 2023.
"Wapinzani wetu Wydad wataingia nchini kesho majira ya saa tano kamili asubuhi hivyo wale wanaohitaji kuwapokea kama ilivyo desturi yetu wafanye hivyo," alisema Ahmed.
Ahmed alisema, waamuzi wa mchezo huo nao wataingia kesho ambapo wanatoka nchi tofauti kama vile Senegal, Ivory Cost, Senegal, Uganda, Afrika Kusini na Misri.