Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wydad ilivyoifanyia Simba Umafia kwa straika huyu

Sidi Bouna Amar Sidi Bouna Amar

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wydad Athletic imeifanyia umafia Simba baada ya kumchukua mshambuliaji Bouna Amar ambaye Wekundu wa Msimbazi walitangulia kumpigia hesabu.

Amar alikuwa mmoja wa mastaa waliofanya vizuri na timu yake ya Taifa ya Mauritania iliyokuwa inashiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zinazoendelea nchini Ivory Coast ambapo Simba ilikuwa imempigia hesabu sambamba na kiungo mmoja wa nchi hiyo.

Wydad ambayo inajisuka upya imemchukua Amar (25) ikiwa kwenye hesabu za kukisuka upya kikosi kilichopungua nguvu msimu huu mara baada ya Mauritania kumaliza ushiriki katika fainali za Afcon.

Amar amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Wydad akitokea klabu ya FC Nouadhibou ya nchini kwao akiwa ndiye staa wa kwanza kusajiliwa chini ya kocha mkongwe, Mtunisia Faouzi Benzarti.

Mchezaji huyo anakwenda kuziba nafasi ya mshambuliaji mkongwe Bouly Junior Sambou aliyetimkia klabu ya Konyaspor ya nchini Uturuki.

Mbali na Sambou, pia Wydad ina kibarua cha kusaka beki mpya baada ya Arsene Zolla naye kuachana na klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live