Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wolves yatibua Krismasi ya Chelsea baada ya miaka 28

Fxftxffc Wolves yatibua Krismasi ya Chelsea baada ya miaka 28

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mambo yanazidi kuwa magumu kwa Chelsea baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Wolves, ugenini kwenye Uwanja wa Molineux na kuendelea kusalia nafasi ya 10 kwenye msimamo. Hicho ni kipigo cha kwanza kwa The Blues kwenye kuamkia Krismasi katika miaka 28 iliyopita zilipokutana mwaka 1995.

Mabao mawili ya Mario Lemina dakika ya 51 na Matt Doherty dakika ya 93, yalitosha kuizamisha Chelsea iliyopata bao la kufutia machozi la nyota wa kimataifa wa Ufaransa, Christopher Nkunku aliyekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha.

Nkunku aliyerejea kwenye mechi ya Kombe la Carabao dhidi ya Newcastle, aliweka kambani bao la dakika za jioni kabisa ya 96 na hivyo kuonyesha amerudi kwenye kazi yake ya kutupia mabao, inayoonekana kuwashinda baadhi ya mastraika wa The Blues wakiongozwa na Armando Broja na Nicolas Jackson.

Hata hivyo, Chelsea itajilaumu yenyewe kwa mabao iliyokosa na Raheem Sterling alishindwa kufunga bao baada ya kubaki na kipa, Jose Sa aliyezuia shuti lake.

Sterling alimfikia kipa huyu baada ya juhudi za kuiba mpira kwa beki wa Wolves, Joao Gomes dakika ya 32.

Chelsea sasa imefikisha mechi 18 ikiwa imeshinda michezo sita pekee, huku ikitoka sare minne na kupoteza nane na ina pointi 22 na mashabiki wa timu hiyo watakula krismasi wakiwa na machungu kwa timu yao hiyo.

Hadi sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, Arsenal inaongoza ikiwa na pointi 40 baada ya michezo 18, ikifuatiwa na Liverpool yenye 39 na vijana wa Mikel Arteta wanakula sikukuu wakiwa kileleni ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo kwani msimu uliopita ilikuwa hivyo, sawa na mwaka 1932 na 1933, ilifanya hivyo ikiwa ni mara mbili mfululizo.

Chanzo: Mwanaspoti