Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wolves waikataa ofa ya Leeds Kuhusu Hwang

Hwang Wolves Hwang Hee-chan

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Wolves imekataa ofa ya Leeds United ambao wameonesha nia yao ya kumsajili mshambuliaji raia wa Korea Hwang Hee-chan.

Leeds bado wanatafuta mtu ambaye anaweza kucheza kwenye safu yao ya ushambuliaji.

Malengo kadhaa yamesalia kufikiwa huku mawasiliano yakifanywa na klabu ya Elland Road na Wolves kuhusu Hwang Hee-chan, mchezaji ambaye aliwahi kufanya kazi na Kocha Jesse Marsch wakati alipokuwa RB Leipzig na Red Bull Salzburg.

Timu hiyo ilisema, hawakupendezwa na pesa zinazojadiliwa na dalili zinaonyesha kuwa timu hiyo watakuwa na ugumu kuwashawishi kumuachia nyota huyo. Kwa mujibu wa BBCSports.

Hata hivyo, kama Leeds hawatapata mojawapo ya chaguo zao ofa hiyo, inaweza kufufuliwa, ambayo inaweza kuwa na athari kwa Dan James, ambaye amevivutia vilabu vingi katika wiki kadhaa zilizopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live