Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wolves mambo magumu, wapanga kumrudisha Nuno Santo

Skysports Nuno Tottenham 5529263 Nuno Espirito Santo

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wolves wanaendelea na mazungumzo na aliyekuwa kocha wao Nuno Espirito Santo ambaye kwa sasa anafanya kazi na klabu ya Saudi Arabia, Al-Ittihad.

Wolves wameanza kumshawishi Nuno, 48, kufuatia kocha raia wa Hispania Julen Lopetegui kuikacha nafasi ya kuwa kocha ndani ya dimba la Molineux.

Licha ya kutofanya vizuri akiwa Spurs, Nuno Espirito Santo bado mashabiki wa klabu hiyo wana mapenzi makubwa na kocha huyo raia wa Ureno.

Wolves wanataka kocha mpya kwa sababu wako kwenye nafasi mbaya ya kushuka daraja kwenye mechi tisa wameshinda mchezo mmoja tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live