Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yatambia maendeleo michezo

Dfrdh Wizara yatambia maendeleo michezo

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa ametambia mafanikio ambayo Tanzania imeonyesha katika michezo miaka ya hivi karibuni.

Akizungumza katika hafla ya kuzichangia timu za taifa inayofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, Msigwa amesema kuwa Tanzania ya sasa ni tishio michezoni.

"Tunamshukuru Rais kwa mchango wake mkubwa kwenye sekta ya michezo. Mafanikio tunayopata hatujawahi kuyapata katika nyakati nyingine zote," amesema Msigwa.

Msigwa amesema kuwa anaipongeza kamati ya hamasa iliyoundwa kwa ajili ya kuhamasisha timu za taifa, imefanya kazi kubwa na anaamini itakuwa na mchango katika maendeleo ya michezo.

"Kamati ya hamasa ina wiki moja lakini imefanya mambo makubwa sana, tumefanya Harambee hii kwa ajili ya kuchagiza maendeleo hayo," alisema Msigwa

Chanzo: Mwanaspoti