Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Michezo yamjibu Eto'o

Samuel Etoo 1 Samuel Etoo, Rais wa Shirikisho la Soka Cameroon

Sat, 6 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika barua iliyotiwa saini na Narcisse Mouele Kombi, Ijumaa Aprili 5, Wizara ya Michezo nchini Cameroon imesisitiza kuwa Kocha Marc Brys ndiye kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Mapema wiki hii, Samuel Eto’o alituma barua kwa Wizara hiyo, akionyesha uharamu wa chaguo la kocha mpya wa Cameroon bila kushirikishwa katika kufanya maamuzi yoyote.

Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot) anaamini kuwa, kwa mujibu wa sheria shirikisho ndilo linalopaswa kuamua hatma ya kocha na benchi la ufundi kwa ujumla.

Samwel Eto’o amekuwa akishutumiwa katika mambo mbali ikiwa ni pamoja na kuingilia majukumu ya kocha na upangaji wa matokeo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live