Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Winga teleza matumaini kibao Ligi Kuu

Enock Atta Agyei Singida Aliyekuwa winga wa Azam FC, Enock Atta Agyei

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa winga wa Azam FC, Enock Atta Agyei amesema bado ana matumaini ya kuichezea Singida Big Stars kwa msimu ujao licha ya Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kucheleweshwa na waajiri wake wa zamani, Horoya AC.

Nyota huyo alijiunga na Singida katika dirisha dogo la Januari ila ameshindwa kuitumikia timu hiyo kutokana na mabosi wa Horoya kuchelewesha ITC yake hivyo kuendelea tu kufanya mazoezi na kikosi hicho hapa Tanzania.

“Naipenda Tanzania na nafurahia nikiwa hapa, natamani ningekuwa nacheza kama wenzangu ingawa matatizo yaliyopo yamenifanya nibaki nje ya uwanja. Naendelea na mazoezi ili kujiweka imara zaidi.”

Akimzungumzia mchezaji huyo Kocha wa Singida, Hans Van Der Pluijm alisema matumaini yake ni kumuona nyota huyo akiichezea timu hiyo kwani ana uwezo wa kucheza namba 10 na 11 kwa ufasaha kwa sababu ni winga halisi.

“Ana spidi uwanjani, anajua kukaa na mpira, ana uwezo wa kuwasumbua wapinzani na kwa kocha yoyote yule asingependa kumpoteza mchezaji wa aina yake hivyo ni suala la muda kwani kila mmoja anatamani uwepo wake.”

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, John Kadutu alisema, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) lilitangaza nyota huyo yuko huru ila changamoto ni kwa timu yake ya zamani ya Horoya kuchelewesha ITC.

“Wanasheria wetu wanalifanyia kazi suala hilo na tuna matumaini atakuwa sehemu ya kikosi chetu ndio maana hadi leo bado tupo naye akiendelea kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti