Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wilson Oruma: Rivers wanajitekenya na kucheka wenyewe

Wilson Oruma Yanga Mchambuzi wa Michezo kutoka kituo cha EFM, Wilson Oruma

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Timu ya Rivers United ikilalamika kupuliziwa Sumu kwenye basi lao na kuibiwa fedha katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Badhi ya wachambuzi na wadau mbalimbali ya Soka wametoa maoni yao kuhusiana na sakata hilo.

Mmojawapo ni Wilson Oruma kutoka E-FM ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Nimeona Malalamiko ya Rivers United Kwamba wameibiwa USD 5,250,Kama nikweli waende Police waka file hili tukio na kuwapa CAF attachment.Lakini kwangu hainingii akilini washushe Vifaa Vyote vya Mazoezi Halafu waache Pesa kwenye gari

Kitu Kingine ambacho nakiona kama ni Uchale chale wa MAPOPOO unapigwaje Dawa saa moja usiku Jana na Mechi ni Leo Saa moja Usiku? Huwa naona ile inapigwa Masaa machache kuelekea Kickoff.Lakini Masaa 24 naona kama ni Mengi mnoo kwa hyo dawa kuendelea kuwa na Nguvu iliyokusudiwa.Wataalam wa Mambo ya chemicals mtanirekebisha hapo if am Wrong.Lakini Kwangu doesn't Make any Sense

Kitu Kingine ni Kusema BUS lao limevunjwa na watu Wameingia Lakini Bila Kuonyesha ushahidi wa Kimazingira.Yani Nimetafuta angalau nione Picha za Kioo Cha Bus lao Kimevunjwa.Hizo Picha mimi Sijabahatika Kuziona,au Labda Kuna mtu ameziona sehemu naziomba .

Halafu Ndugu zangu RIVERS UNITED Unapigwaje Dawa hapa Lupaso wakati Umeshachukua 2-0 sebuleni kwako? Au hata pale Goodwill AKPABIO ulipigwa Dawa? Huu Kwangu naona kama ni Uchale chale Mwingine

Mwisho ni kwa Ndugu Wanahabari Kutoka Tanzania, Uzalendo wenu upo Wapi? YANGA AFRICA ndo Mwakilishi wetu pekee Africa Mashariki na Kati amebaki kwenye Mashindano ya CAF.Tunachukuaje habari Kutoka Nigeria na Kuiripoti kwa Wingi wakati sisi wenyewe Watanzania tupo hapa hapa?

Mimi Ugomvi Wangu Mkubwa na Haji Manara kama mlikuwa hamjui ulianza baada ya yeye Kuripoti kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwapa taarifa ASEC MIMOSAS kwamba wawe makini na Simba Sports huwa wanapuliza dawa kwenye AC za Dressing room.Nikamcharaza sana nikamwambia yeye kuripoti vile inamsadia Nini??

Sisi Watanzania tuna USHAMBA flani hivi.Hivi mnafikiri hii taarifa Ingetokea nchini Nigeria ikifanywa na Yanga Africa,vyombo vya habari nchini Nigeria vingeishadadia kama Sisi tunavyofanya sasa hivi?

Tupunguze USHAMBA na SHOBO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live