Uongozi wa klabu ya Simba, jana umemtambulisha kiungo mshambuliaji wa kimataifa, Willy Essomba Onana (23) raia wa Cameroon kwa mkataba wa miaka miwili.
Onana amesajiliwa kutoka Rayon Sports ya Rwanda ambapo msimu uliopita aliibuka mchezaji bora wa ligi kuu nchini humo.
Mchezaji huyo ndiye ingizo jipya la kwanza kwenye kikosi cha Simba ikiwa ni sehemu ya maboresho kuelekea Msimu mpya wa Ligi 2023/24.
Ni kweli wakati Michael Sarpong anasajiliwa na Yanga alitoka kuwa mchezaji bora (MVP) wa Ligi Kuu ya Rwanda na mfungaji bora akiwa na magoli 16.
Simba wamemsajili Onana akiwa MVP wa Rayon Sports na mfungaji bora wa kikosi hicho akiwa na magoli 16.
Je, Onana ni kama Sarpong? Jibu ni ndio au hapana. Kwanini?
Kwanza ni wachezaji wawili tofauti. Pili, kushindwa kwa Sarpong hakutafsiriwi moja kwa moja kwamba alitoka kucheza ligi dhaifu (Rwanda) ndio maana akafunga mabao 16.
Kumbuka kwamba, timu dhaifu hutoa wachezaji wazuri ndio maana licha ya Marumo Gallants kushuka daraja Mabingwa wa ligi hiyo Mamelodi Sundowns wamemsajili Wiliam Lesiba Nku, Otladisa kaenda Orlando Pirates na Ranga Chivaviro kaenda zake Kaizer Chiefs.
Ligi dhaifu pia hutoa wachezaji wazuri.
Ligi ya Zanzibar tunayoiona ya kawaida ndio ametokea Feisal Salum, Ibrahim Bacca, Nadir Haroub, Mudathir Yahaya na wengine, lakini pia ndio ametoka Bashima Sauli Saite na wengine.
Ligi anayocheza Wiliam Saliba ndio ligi hiyo hiyo anacheza Harry Maguire, hivyo basi, Onana anaweza kufanya vizuri kama atapewa muda na anaweza kuwa Michael Sarpong vilevile kama uwezo wake ni mdogo.
Lakini nakuacha na swali dogo tu kwamba, Simba wanatafuta Ubingwa wa CAF Champions League kwa kusajili Rayon Sports?