Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Willian kutimkia Saudi Arabia

Willian Fulham Willian kutimkia Saudi Arabia

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Willian ana kipengele katika mkataba wake na klabu ya Fulham ambacho kinaweza kumfanya aondoke bila malipo msimu huu wa joto ikiwa ni majuma machache tu, baada ya Mbrazil huyo kuongeza mkataba mpya.

Willian anaweza kuwa njiani kuondoka baada ya klabu ya Al-Shabab ya Saudia kutoa ofa ya kumsaini, ambayo ni kubwa zaidi na hii ni kwa sababu ya kifungu cha siri katika mkataba wake ambacho kinasema kwamba, ikiwa atapata ofa kubwa ya kifedha nje ya kawaida anaweza kuondoka Fulham bure, kulingana na ripoti ya Premier League Brasil.

Timu hiyo kutoka Saudi Pro League imempa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Pauni 200,000 kwa juma, ambayo ni mara mbili ya kiasi anachopata Fulham kwa sasa.

Willian tayari ameripotiwa kukubaliana na Al-Shabab na amemwambia Marco Silva angependa kuondoka na kuanza safari mpya Mashariki ya Kati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live