Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Willian arejea EPL

Wili Pic Data Willian

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Fulham imemsajili nyota wa zamani wa Chelsea na Arsenal Willian, 34, pamoja na mshambulizi wa zamani wa Tottenham Carlos Vinicius, 27 masaa machache tu kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Willian, alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka katika klabu ya Corinthians kutoka  Brazil, baada ya mkataba wake kuisha msimu uliopita na amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Fulham.

Kabla ya Willian kusajiliwa na Fulham alikuwa akifanya mazoezi ndani ya viunga hivyo. akizungumza baada ya kutua kiungo huyo Mbrazil amesema ana furaha kubwa kurejea Ligi Kuu England baada ya kuondoka.

“Nina furaha kuwepo hapa, nina furaha kurejea Ligi Kuu,  Fulham ni klabu nzuri, imeonyesha ipo tayari kuleta changamoto, nitahakikisha ninatoa mchango wangu kuhakikisha timu inafikia malengo," alisema Willian.

Mkongwe huyo ataongeza ubunifu na uzoefu aliyokuwa kikosini kwani aliwahi kupata mafanikio na amebeba mataji mawili ndani ya kipindi cha miaka saba alipokuwa akikipiga Chelsea, Willian aliichezea jumla ya mechi 339,  na kufunga mabao 63 kabla ya kuhamia Arsenal.

vilevile Fulham imekamilisha uhamisho wa Daniel James aliyejiunga akitokea Leeds United, Layvin Kurzawa aliyetua kwa mkopo wa msimu mzima akitokea Paris Saint-Germain.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz