Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wilfried Zaha Kuiwakilisha Ivory Coast AFCON

Zaha Wilfried Zaha

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa timu ya Crystal Palace Wilfried Zaha ameitwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast ambayo inatarajia kushiriki mashindano ya AFCON mwezi January 2022.

Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 29, mwezi Novemba alikataa kujiunga na timu yake ya taifa kwa sababu ya kuwa kila alipokuwa anakuja kuiwakilsha timu yake ya taifa alikuwa anapata maradhi, lakini kocha wa Ivory Coast Patrice Beaumelle amemjumuisha kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya AFCON Januari.

Timu ya Ivory Coast inatajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa ufungunzi kwenye kundi lake Januari 12 huku ukifuatiwa na mchezo wa Sierra Leone dhidi ya Algeria.

Zaha ambaye imeifungia timu ya ivpry coast magoli 20 anakwenda kuungana na Eric Bailly wa Manchester United, Willy Bolly wa Wolves, Maxwell Cornet wa Burnley na Nicolas Pepe wa Arsenal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: