Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wiki ngumu kwa Simba ikiisubiri AS Vita

SIMBAAA Wiki ngumu kwa Simba ikiisubiri AS Vita

Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

RATIBA ya Shirikisho la soka Afrika linaonyesha timu za taifa zitamaliza mechi zake Machi 30, na kila mchezaji kurejea katika majukumu ya klabu yake.

Wakati huo huo ratiba ya CAF, inaonyesha Simba wanatakiwa kucheza mechi ya mzunguko wa tano Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Aprili 3, muda mchache mara baada ya wachezaji kutoka katika majukumu ya timu za taifa.

Kocha wa Simba, Didier Gomes alisema ratiba imekuwa ngumu mno ila bahati nzuri hawataathirika pekee yao bali hata klabu nyingine ambazo zinacheza mashindano hayo ya kimataifa.

Gomes alisema katika timu za taifa anawachezaji 19, na msaidizi wake, Selemani Matola ambao wengi wao watakuwepo kambini kuanzia Aprili 1, siku mbili kabla ya kucheza mchezo huo mgumu.

"Niangalie kwa upande wetu mchezaji kama Luis Miquissone anaweza kuwepo hapa nchini siku moja kabla ya kucheza na AS Vita, wakati huo huo hawatakuwa na muda wa kutosha kufanya maandalizi ya pamoja na kuangalia namna gani tutawakabili wapinzani," alisema.

"Haina jinsi kutokana na ugumu wa ratiba hiyo ilivyo tutafanya darasa na wachezaji wangu na mazoezi mepesi jioni siku moja kabla ya mechi ili kuona namna gani tutakwenda kukabiliana nao AS Vita," alisema.

Related Gomes akomaa na mastaa 10 Chikwende aipeleka Zimbabwe Afcon Tizi la kina Morrison, Mugalu ni balaa!"Unajua mechi hii ndio inaamua hatma yetu ya kucheza robo fainali kwahiyo tunatakiwa kupata ushindi ili kuwa na uhakika huo, lakini AS Vita nao watakuja kutaka pointi kutoka kwetu kama ambavyo tulifanya kwao.

"Kama tungepata muda wa kutosha maana yake tungeweza kuweka mipango yetu mingi sawa tukiwa kwa pamoja lakini haina jinsi kutokana na mazingira yalivyo tutaandaa timu ili kwenda kuvuna pointi tatu katika mechi hiyo," alisema Gomes.

Katika hatua nyingine Gomes alisema jambo zuri katika kikosi chake wengi wa wachezaji wapo katika timu ya Taifa Stars ambao mechi ya mwisho wanamalizia hapa nyumbani na mara baada ya mchezo wataingia kambini haraka.

Gomes alisema baada ya kuona ugumu huo wa ratiba ya CAF, tumeanza maandalizi ya mapema kwa wachezaji tuliobaki nao kuwapa mazoezi mengi ya kutosha ili watakapoungana na wenzao kuwa sawa katika utimamu wa mwili na hali ya ushindani.

"Wachezaji waliokuwa katika timu za taifa wanafanya mazoezi naimani wanajitambua na wanaelewa majukumu ya kazi yao wakija kuunganisha nguvu na hawa waliobaki hapo nitawaelekeza cha kwenda kukionyesha katika mchezo huo ambao naimani tutafanya vizuri kutokana na faida ya kuwa nyumbani," alisema Gomes.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz