Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Westham wamefuta ndoto za Liverpool kutwaa ubingwa?

Liver Sare.jpeg Je ushindi wa Westham dhidi ya Liverpool wikendi unaipa matumaini kushinda taji la ligi ya Premier?

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

West Ham iliilaza Liverpool baada ya kupata ushindi mkubwa ambao uliwasaidia kupanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya premia mbali na kutia doa matumaini ya klabu hiyo kushinda taji la ligi.

Liverpool ilianza mechi hii ikiwa na lengo la kuimarisha rekodi yake ya kutofungwa kufikia mechi 26, mbali na kupata ushindiambao ungewapeleka hadi katika katika nafasi ya pili wakiwa pointi moja nyuma ya viongozi Chelsea

Lakini walijipata nyuma mapema , wakati Alisson , akiwa chini ya shinikizo kutoka kwa Angelo Ogbonna, alipangua kona iliopigwa na Pablo Fornal na kujifunga.

Pande zote mbili baadaye ziliipuka kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza huku Aaron Cresswell akimchezea visivyo Jordan Henderson kabla ya Ogbonna kupigwa kisukusuku na Diogo Jota – suala lililomfanya beki huyo wa Westham kutolewa nje.

Mechi hiyo ilikamilika huku West Ham wakiilaza Liverpool 3-2.

Na walipoulizwa iwapo wanaweza kushinda taji , walijibu

‘’Hatujui , ni mapema mno . lakini iwapo tutapigania ushindi katika kila mechi kama tulivyofanya hii leo kwanini tusiwe na ndoto ya kushinda’?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live