Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

West Ham wampa Ofa ya Mkataba wa Miaka 8 Declan Rice

Rice Kiungo wa West Ham na England, Decline Rice

Thu, 12 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika harakati za kuhakikisha wanasalia na kiungo wao, Klabu ya West Ham wamempa ofa ya mkataba mpya wa miaka 8 kiungo wake na kapteni wa klabu Declan Rice.

Mkataba huo mpya utamfanya Rice, 23 kuvuta kiasi cha £200,000 kwa wiki mpaka mwaka 2030, ili kuepusha mchezaji huyo kuondoka baada ya kuhusishwa kuondoka.

Klabu za Manchester united na Chelsea zimekuwa zikihusishwa na mchezaji huyo wa West Ham aliyegoma kuongeza mkataba mpya miezi kadhaa iliyopita.

Rice ameichezea West Ham mechi 48 katika mashindano yote msimu huu akifunga magoli matano na kusaidia upatikanaji wa magoli mengine (assist) manne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live