Klabu ya West Ham imezuiwa kuuza tiketi kwenye mchezo wao wa unaofuata wa nyumbani kwenye michuano ya UEFA Europa League kutokana na mashabiki wao kufanya fujo kwenye mchezo waliosafiri kwenda Genk.
Pia klabu ya West Ham imepigwa faini ya kiasi cha euro 34,500 kutokana na vurugu zilizosababishwa na mashabiki wao nchini Ubelgiji kwenye mchezo uliosha kwa sare ya 2-2 tarehe 4 November.
Kulingana na waraka uliotolewa na UEFA, West Ham United hawataruhusiwa kuuza tiketi na watalipa faini ya kiasi cha euros 30,000 ni kutokana na vurugu walizosababisha mashabiki wao na nyongeza ya euros 4,500 hii ni kwa ajili kurusha vitu kwa mashabiki waliosafiri.
West Ham watasafiri kwenda jijini Rapid Vienna kwenye mchezo wa Europa League tarehe 25 novemba baada ya michezo ya kimataifa kuisha.