Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

West Ham waipiku Brighton dili la Kudus

Ajax Man Mohammed Kudus Mohamed Kudus

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbali ya Brighton, West Ham pia inatajwa ni timu nyingine kutoka England inayohitaji huduma ya kiungo wa Ajax, Mohammed Kudus katika dirisha hili na inataarifiwa kuwa iko katika hatua nzuri kuliko wapinzani wao Brighton.

West Ham inataka huduma ya fundi huyu kama mbadala wa staa wao kutoka Brazil, Lucas Paqueta, 25, anayehusishwa na Manchester City.

Kudus anadaiwa kuomba kuondoka Ajax kwenye dirisha hili na huko nyuma aliwahi pia kuhusishwa na Manchester United akajiunge na Kocha Eric Ten Hag.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live