Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Werder Bremen wamsimamisha Naby Keita mpaka mwisho wa msimu

Naby Keita Ujerumani Naby Keita

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Liverpool, Naby Keita amesimamishwa na klabu yake ya Werder Bremen mpaka mwisho wa msimu baada ya kudaiwa kugoma kusafiri na timu hiyo kuelekea mchezo wao dhidi ya Bayer Leverkusen uliomalizika kwa kipigo cha 5-0.

Nyota huyo raia wa Guinea alifikia uamuzi wa kugoma kusafiri na timu baada ya kubaini kuwa hakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kilichoanza dhidi Mabingwa hao wapya wa Bundesliga.

Keita 29 ameichezea Werder Bremen mechi tano msimu huu huku akianza mara moja tu akiwa amecheza jumla ya dakika 106 kwenye Bundesliga.

Keita amekuwa akikabiliwa na majeraha msimu huu lakini aliichezea Guinea mara nne kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live