Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema huenda The Gunners wasipate nafasi nzuri ya kushinda Ligi ya Primia na amewaonya kabla ya mchezo wao wa kesho dhidi ya Manchester City.
Wenger aliiwezesha Arsenal kutwaa mataji matatu ya Ligi ya Primia, lakini The Gunners hawajamaliza wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza tangu mara ya mwisho kati ya ushindi huo katika kampeni za 2003-04.
Hata hivyo, huku Mikel Arteta sasa akiwa ameshikilia usukani, timu hiyo ya London iko pointi tatu mbele ya City inayoshika nafasi ya pili ikiwa na mchezo mkononi kuelekea mchezo wao wa Emirates.
Arsenal wamekuwa na kigugumizi hivi karibuni, wakichukua pointi moja pekee kutoka kwa mechi zao mbili zilizopita, na kocha maarufu wa zamani Wenger amewataka wasiruhusu fursa hiyo kupita kwao.
“Ninakubali hali ya msimu ujao haitakuwa nzuri kama ilivyo sasa, kwa hivyo tusikose fursa hii. Arsenal wana alama 51 baada ya michezo 21, ambayo ni ya kushangaza. Ninahisi vitisho vya kawaida vyote viko nje ya mbio. Tishio pekee ni City na hata City sasa sio kubwa kama ilivyokuwa mwaka jana au miaka miwili kabla.”
Wenger alijiuzulu kama kocha wa Arsenal Mei 2018 baada ya miaka 22 katika kazi hiyo, ambapo alishinda tuzo kuu 10.
Mfaransa huyo alirejea kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Emirates kwa Arsenal kushinda 3-1 dhidi ya West Ham siku ya Boxing Day, lakini alikuwa na hisia tofauti baada ya kukaa kwa muda mrefu katika klabu hiyo.
Wenger amesema; “Nilitaka kuipeleka familia yangu huko na nadhani ni mwisho wa sura. Nilifurahi kuwaona wachezaji kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Ilikuwa hisia mseto. Nilitoka jasho kujenga uwanja huu kwa miaka 10 au 12, kila senti. Ilikuwa ni hisia nzuri kuona ilivyo sasa huku umati wa watu ukifurahia timu inafanya vizuri.”
Arsenal wamepoteza mechi 10 zilizopita za Primia Ligi dhidi ya City, ukiwa ni msururu wao mrefu zaidi wa kupoteza dhidi ya wapinzani wao katika historia ya ligi.