Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenger ajutia kuchelewa kuondoka Arsenal

1917 Arsene Wenger 1 Wenger ajutia kuchelewa kuondoka Arsenal

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: Nipashe

ARSENE Wenger anajutia kung’ang’ania kubaki kwenye Klabu ya Arsenal baada ya kuondoka kwa uchungu msimu wake wa mwisho mwaka 2018.

Wenger mwenye umri wa miaka 72, aliitumikia klabu ya Arsenal kwa muda wa miaka 22 na kuiongoza kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu England na mataji saba ya Kombe la Ligi, FA.

Kuna makala imeandaliwa ya msimu wa 2003/04 ambayo imepewa jina la “Arsene Wenger: Invincibles” na inatarajiwa kutoka wiki hii na kuonyeshwa kwenye kumbi mbalimbali za sinema.

Wenger ameweka wazi kuwa ilibidi aondoke Arsenal miaka kumi iliyopita, wakati anahitajika na klabu nyingi pamoja na timu za taifa.

Wenger amesema, “muda mwingine nashang’aa, kuna kitu nilikosea baada ya msimu wa “Invincible” 2003/04?

“Mwaka 2007 ulikuwa ni wa maamuzi, ni kwa mara ya kwanza nilihisi kuwa kuna msukumo mkubwa ndani ya bodi, ilikuwa nichague kuwa mwaminifu kwa klabu au vinginevyo.

“Bado nashang’aa, kama nilifanya kitu sahihi, kwa sababu maisha hayakuwa kama yalivyokuwa baadaye. Nadhani, muda wa kumaliza mradi ulikuwa umefika.

“Ningeweza kwenda kuifundisha timu ya Taifa ya Ufaransa, timu ya Taifa ya Uingereza mara mbili au tatu, ningeweza kwenda Real Madrid, ningeweza kwenda Juventus, Paris Saint Germain hata Manchester United.”

Chanzo: Nipashe