Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenger: Siasa zimewaponza Ujerumani

Wenger Arsene Wenger atoa sababu za Ujerumani kuboronga Qatar

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema chanzo cha timu ya taifa ya Ujerumani kutolewa mapema kwenye michuano ya kombe la dunia inachangiwa na timu hiyo kujiingiza kwenye maandamano ya kisiasa.

Ujerumani wametolewa kwenye Michuano ya Kombe la dunia kwa mara ya pili mfululizo baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye kundi na kukusanya jumla ya alama nne sawa na Hispania lakini wakizidiwa kwa idaidi ya magoli.

Mechi ya kwanza ambayo Ujerumani walipoteza walipiga picha ya kufunika mdomo kuonesha ishara ya kupinga maamuzi ya nahodha wao Manuel Neuer kuzuiwa kuvaa kitambaa cha unahodha chenye alama ya One Love ikimaanisha kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja wakati Qatar imezuiliwa.

Timu hiyo ilionesha imejiingiza kwenye maandamano ya kisiasa jambo ambalo kocha wa zamani wa Arsenal ambaye kwasasa ni mkuu wa kitengo cha utafiti Fifa alizungumza “Timu ambazo zina uzoefu wa kucheza mechi za kombe la duni kama Ufaransa na Uingereza zilishinda mechi zao za kwanza. Na timu hizo ni timu ambazo zilikua tayari kiakili na sio maandamano ya kisiasa”

Mbali na kocha huyo wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger pia mchezaji wa klabu ya Real Madrid alizungumza siku kadhaa nyuma kua wachezaji wa Ujerumani wamevurugwa kiakili baada ya kujiingiza kwenye kampeni za kisiasa ambazo hawakutakiwa kujiingiza kama wachezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live