Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa Saudia Arabia amtaka Ronaldo

Skysports Cristiano Ronaldo 5823297 Waziri wa Saudia Arabia amtaka Ronaldo

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Michezo wa Saudi Arabia, Prince Abdulaziz bin Turki Al-Faisal amebainisha nia ya kutamani kumuona Cristiano Ronaldo akishiriki katika Ligi Kuu ya Nchi hiyo kufuatia kuvunjiwa mkataba wake na Klabu ya Manchester United.

“Nani ambaye hatamtaka Ronaldo kucheza kwenye Ligi yetu? Ni mfano wa kuigwa kwa vijana wengi sana duniani, yeye na Messi ningependa kuwaona wote kwenye Ligi yetu, wachezaji wakubwa.

Hiyo itasaidia kuonesha namna gani Ligi yetu inakua na kipi tunakifanya katika kuhakikisha tunaleta maendeleo kwenye michezo.” alisema Prince Abdulaziz bin Turki Al-Faisal.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amegusia uwezekano wa wawekezaji ndani ya nchi yake kuwekeza kwa kununua klabu za Manchester United pamoja na Liverpool ambazo kwa sasa zipo sokoni.

Amebainisha kuwa klabu za Manchester United pamoja na Liverpool zinaendelea kufanya vizuri kutokana na kuwa na mtaji mkubwa wa mashabiki na wanachama duniani.

Kwa hiyo ikitokea kama wawekezaji wa Saudi Arabia wakapewa nafasi ya kununua vilabu hivyo basi itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza maendeleo ya soka nchini Saudi Arabia kwa kubadilishana uzoefu kwa mataifa hayo.

Amesisitiza kuwa hadi sasa Saudi Arabia inashirikiana vizuri na klabu ya Newcastle United ya nchini Uingereza ambayo inamilikiwa na Tajiri kutoka nchini Saudi Arabia

Chanzo: www.tanzaniaweb.live