Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa Michezo Ivory Coast kwa Mkapa kumshuhudia Pacome

Pacome Chama Pc Pacome Zouzoua.

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast, Adjé Silas ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili kuhusu ushirikiano wa nchi hizo kwenye Sekta ya michezo ambapo Ndumbaro amemualika Silas kushuhudia mechi ya Derby ya Kariakoo (Yanga SC na Simba SC) itakayochezwa kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mechi hiyo Waziri huyo atawaona wachezaji nyota wa timu hizo akiwemo mchezaji Pacome Zouzoua wa Yanga SC ambaye ni raia wa Ivory Coast.

Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pia atashiriki hafla ya kuingia makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ivory Coast katika sekta ya michezo itakayofanyika Aprili 21, 2024 Jijini Dar Es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live