Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ndumbaro aikaribisha Al Ahly kujenga Akademi Tanzania

Ndumbarooooooooooooo Waziri Ndumbaro aikaribisha Al Ahly kujenga Akademi Tanzania

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro ameikaribisha klabu ya Al Ahly ya Misri ije kuwekeza katika sekta ya michezo nchini Tanzania kwa kufungua akademi ya michezo ili kukuza na kuendeleza vipaji vya wanamichezo.

Dk Ndumbaro ameikaribisha klabu hiyo namba moja Afrika hivi karibuni alipofanya ziara kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa na timu hiyo katika jiji la Cairo, nchini Misri.

Timu hiyo pia inamiliki kituo cha Gezira Center ambacho kinaendesha viwanja vya michezo mbalimbali ikiwemo soka, mpira wa wavu, mpira wa netiboli, gofu na riadha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live