Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu awapongeza Yanga kuichapa Marumo

KIKOSI JEZI NYEUSI YANGA 1140x640 Waziri Mkuu awapongeza Yanga kuichapa Marumo

Thu, 11 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukubwa na ubora Yanga unaendelea kuonekana kila kona hapa nchini, baada ya jana timu hiyo kutawala bungeni jijini Dodoma leo hii simulizi ya timu hiyo inaendelea kutawala bungeni.

Akizungumza wakati wa kipindi cha maswali majibu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza timu hiyo kwa kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa baada ya jana kutakata kwenye Dimba la Benjamini Mkapa kwa kuisulubisha Marumo Gallants bao 2-0 kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

"Hakika Dar Young Africans inaendelea kupuperusha vyema bendera ya Tanzania, na niwapongeze sana kwa maatokeo ya jana, tunawaombea sana kwa mchezo wa marudiano kule Afrika Kusini mshinde kwa magoli mengi, Watanzania tuna hamu ya kuona tukishiriki fainali,” alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Majaliwa amesema taifa linajivunia ubora wa timu hiyo na imani yao ni kwamba bendera ya taifa itaendelea kuwakilisha vyema na mabingwa hao wa LKB.

Aidha, Waziri Mkuu amesema shauku ya serikali ni kuiona timu hiyo ikicheza fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live