Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu aridhishwa na ukarabati uwanja wa Benjamini Mkapa

Waziri Mkuu Aridhishwa Na Ukarabati Uwanja Wa Benjamini Mkapa Waziri Mkuu aridhishwa na ukarabati uwanja wa Benjamini Mkapa

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 4,2023, amekagua ukarabati unaoendelea katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, ikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kuanza kwa michuano ya African Football League.

Majaliwa amejionea jinsi maeneo mbalimbali ya uwanja huo yanavyoendelea kufanyiwa ukarabati.

"Nisime tu nimeridhishwa na ukarabati na ninaamini kwamba mechi ya kwanza ya ufunguzi ya Simba SC dhidi ya Al Ahly itakwenda kufanyika ukiwa umekamilika," alisema Waziri Mkuu.

Katika ukaguzi huo Waziri Mkuu ameongozana na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro pamoja na viongozi mbalimbali.

Uwanja wa Mkapa utatumika katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya African Football League ambapo Simba itacheza dhidi ya Al Ahly ya Misri Oktoba 20 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live