Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mchengerwa atembelea klabu ya Fenerbahche-Uturuki

MCHENGERWA 1080x640.jpeg Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: dar24.com

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametembelea moja ya klabu kongwe na mashuhuri duniani, Fenerbahche ya Uturuki, na kukubaliana kushirikiana katika maeneo ya mafunzo, kambi na ujenzi wa shule za michezo.

Akizungumza katika kikao kilichoongozwa na Mjumbe wa Bodi ya Klabu hiyo anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bw. Bekir Irdem, Waziri Mchengerwa pia ameishukuru klabu hiyo kwa kuwahi kuwa na mchezaji kutoka Tanzania, Mbwana Sammatta, na kuikaribisha klabu hiyo kuja kuweka kambi ya msimu mpya mwakani nchini Tanzania.

“Leo tu baadae tutakuwa na kikao cha Bodi na nitawasilisha mapendekezo haya ili tuweze kuanza ushirikiano wetu mara moja,” aliahidi Bw. Irdem.

Katika ziara hiyo Mhe. Mchengerwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Lt. General Yacoub Mohammed na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi.

Chanzo: dar24.com