Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Junior aahidi kuvaa viatu vya Bocco

Waziri Junior Aahidi Kuvaa Viatu Vya Bocco Waziri Junior aahidi kuvaa viatu vya Bocco

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa @kmcfc_official @wazir_junior_10 amesema yupo tayari kuvaa viatu vya mshambuliaji mkongwe John Bocco na kufanya yale aliyokuwa akifanya mchezaji huyo wa @simbasctanzania.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa kesho Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ambapo amesema yeye ni moja wa washambuliaji watakaorithi mikoba ya Bocco huku akiwataka washambuliaji wengine kuhifadhi takwimu zao.

Mpaka sasa Waziri amefunga mabao 50 kwenye Ligi Kuu akiwa amehudumu kwenye vilabu Saba katika misimu 9 aliyocheza kwenye ligi hiyo namba sita kwa ubora Afrika.

Nyota huyo mwenye mabao 11 kwenye ligi msimu huu amesema idadi ya mabao aliyofunga yanampa kila sababu ya kuamini ana uwezo wa kuvaa viatu vya Bocco na kusisitiza kuwa anaheshimu makubwa aliyoyafanya akiwa Azam Fc ,Simba na Taifa Stars.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live