Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Jr, Moalin kizungumkuti, TFF kimya

Waziri Junior Kmc Waziri Jr, Moalin kizungumkuti, TFF kimya

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kumtambulisha mchezaji bora wa mwezi Septemba katika Ligi Kuu, mshambuliaji wa Kmc, Waziri Junior bado hajapata tuzo yoyote ile hadi sasa ikiwa imebaki siku moja tu kuingia mwezi Novemba.

Waziri Junior alichaguliwa mchezaji bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu msimu 2023/24 na kuwashinda Jean Baleke wa Simba na John Nakibinge wa Tabora Utd ambao aliingia nao fainali.

Taarifa ya bodi ya Ligi Kuu iliyotolewa Oktoba 5,2023 ilieleza;"Kwenye mchakato wa tuzo za mwezi uliofanya na kamati ya tuzo za Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Waziri alifunga mabao mawili katika michezo miwili ilicheza Kmc."

Upande wa kocha, tuzo hiyo ilichukuliwa na kocha mkuu wa KMC, Abdihamid Moalin akiwashinda Roberto Oliveira wa Simba na Abdallah Mohammed wa Mashujaa.

Mwananchi lilifatilia wawili hao kwa kina katika mechi zote tatu ambazo timu hiyo ilicheza na kuona wazi hakuna sehemu ambapo walipopewa sehemu ya zawadi zao (King'amuzi).

Oktoba 7, Kmc ikiwa nyumbani ilicheza dhidi ya Ihefu katika uwanja wa Uhuru, ikacheza ugenini dhidi ya Tabora United (Oktoba 22) na juzi Oktoba 27, ilicheza katika uwanja wake wa nyumbani Uhuru dhidi ya Tanzania Prisons lakini bado kocha wala mchezaji huyo hawakuonekana wakipewa tuzo zao.

Mwananchi halikuishia hapo kwani lilichimba hadi ndani ya KMC na lilipenyezewa kwamba bado wawili hao hawajapewa hata zawadi ya fedha kiasi cha Sh 1 milioni ambayo inatoka kama sehemu ya fedha.

"Bado hawajapata, nadhani bado mambo hayajakaa sawa, tusubili tu,"kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa ofisa habari wa bodi ya Ligi, Karim Boimanda alisema kama tuzo imechelewa kwa mchezaji wa timu ya mkoani mara nyingi hupewa anapokuwa na mchezo wa hapa Dar es Salaam lakini kama ni wa hapa na hajapewa basi waulizwe watu wa kamati ya mashindano.

"Kuna muda ni ngumu mtu wa bodi kusafiri na kwenda kumpa tuzo mkoani lakini anapokuja kuucheza hapa basi anapewa tuzo yake (King'amuzi),"alisema Boimanda.

Alipotafutwa mwenyekiti wa kamati ya tuzo TFF, Ahmed Mgoyi alisema kwa kifupi;"Mtafute Ndimbo yeye ndio anazungumzia masuala yote."

Ndimbo alipopigiwa simu alikata na kutuma ujumbe mfupi kwamba yupo kanisani.

"Nipo kanisani, nikitoka nitakupigia,"aliandika Ndimbo.

Chanzo: Mwanaspoti