Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazir Junior atua kwenye rada za Ihefu

Waziri Jr Kk Waziri Junior

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kama mambo yakienda sawa, mshambuliaji aliyemaliza mkataba wake KMC, Waziri Junior anaweza akasaini muda wowote kuanzia leo Jumanne, baada ya kurejea kutoka katika majukumu ya Taifa Stars.

Mmoja wa kiongozi wa Ihefu, alisema kila kitu kuhusu Junior kinakwenda vizuri, walikuwa wanamsubiri arejee kutoka katika majukumu ya timu ya taifa 'Taifa Stars', ambayo ilikwenda nchini Indonesia.

"Kabla ya kuitwa timu ya taifa, tulishafanya naye mazungumzo, ilibakia kusaini, hivyo kila kitu kinaweza kikakamilika muda wowote kuanzia sasa," alisema.

Ligi Kuu Bara iliyoisha, Junior alimaliza na mabao 12, jambo lililowavutia viongozi wa Ihefu, kuona anawafaa kuwa sehemu yao msimu ujao.

Lakini alipotafutwa Junior, ili kuthibitisha hilo alisema "Ni suala la muda, mchezaji anacheza eneo la wazi, hivyo mtajua tu, msimu ujao nitaichezea timu gani."

DATA ZAKE

Msimu wa 2015/16 akiwa na Toto Africans, mabao saba, 2016/17 (Toto) mabao 7, 2017/18 bao moja (Azam FC), 2018/19 (Biashara United) mabao matatu, 2019/20 mabao 13 (Mbao FC) pray-off mabao 2, 2020/21 mabao mawili (Yanga), 2021/22 mabao manne (Dodoma Jiji), 2022/223 bao moja (KMC) na 2023/24 mabao 12 (KMC).

Chanzo: Mwanaspoti