Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazir Jr ni sawa na mastraika sita Simba,Yanga

Waziri Jr Kk Straika wa KMC, Waziri Jr

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ukichubgulia ‘Top ten’ ya vinara wa mabao Ligi Kuu hadi sasa utagundua viungo na mawinga wameteka chati hiyo.

Washambuliaji asilia (namba tisa) kwenye orodha hiyo ni watatu, Wazir Junior wa KMC mwenye mabao 11, Prince Dube wa Azam na Samson Mbangula tu, ambao kila mmoja ana mabao saba.

Hata hivyo, msimu huu umekuwa bora kwa mshambuliaji Wazir Junior kwani anashika nafasi ya tatu kwa upachikaji mabao nyuma ya viungo Stephane Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum wa Azam wanaoongoza kila mmoja akiwa amecheka na nyavu mara 12.

Waziri ameonyesha utofauti na mastraika wengine lakini kubwa zaidi amefunga mabao 11 ambayo ni moja pungufu kwa mabao 12 waliyofunga mastraika sita asilia waliopo Simba na Yanga hadi sasa.

Mastraika asilia wa Simba ni John Bocco, Pa Omar Jobe na Freddy Michael huku kwa Yanga wakiwa Clement Mzize, Kennedy Musonda na Joseph Guede ambao kwa pamoja wamefunga mabao 12 tu kwenye ligi hadi sasa.

Kwa Yanga, Mzize na Musonda ndio mastraika asilia waliofunga mabao mengi kwenye ligi kila mmoja akifunga matatu huku Joseph Guede akiwa bado hajacheka na nyavu kwenye ligi.

Upande wa Simba Freddy ndiye anaongoza akiwa na mabao matatu kwenye ligi akifuatiwa na John Bocco mwenye mawili huku Pa Omar Jobe akiwa nalo moja tu.

Chanzo: Mwanaspoti