Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazir Jr kurejea tena Dodoma Jiji

Waziri Jr Goals Wazir Junior

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji mzawa aliyemaliza na mabao 12 katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Wazir Junior Shentembo yupo katika mazungumzo ya kutaka kurejea tena Dodoma Jiji akitokea KMC.

Inadaiwa mabosi wa Dodoma wapo hatua za mwisho za kukamilisha dili hilo la nyota huyo wa zamani wa Toto Africans, Yanga na Mbao FC.

Awali, nyota huyo alikuwa akipigiwa hesabu na klabu za Singida Black Stars na Pamba Jiji zilizoonyesha nia ya kumhitaji, kabla ya Dodoma Jiji kuingilia kati na muda wowote huenda jamaa akaibukia kwenye timu hiyo aliyowahi kuitumikia kabla ya kutua KMC.

Wazir amekuwa na msimu mzuri uliopita wa Ligi Kuu Bara akiwa ndiye mshambuliaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika ligi nzima katika msimu ambao ulitawaliwa na viungo, Stephane Aziz Ki wa Yanga akimaliza mfungaji bora kwa kufunga mabao 21, akifuatiwa na Feisal Salum 'Fei Toto' wa Azam (mabao 20). Kisha wa tatu akawa Wazir Jr, akiwa mshambuliaji pekee kwenye Top 3.

Daudi Elibahati

WAZIR JUNIOR

Kuzaliwa: Jan 08, 1996

Mahali: Nyamagana, Mwanza

Nchi: Tanzania

Nafasi: Mshambuliaji

Klabu: KMC

Alikopita: Toto Africans, Azam FC, Biashara Unitd, Mbao, Yanga, Dodoma Jiji

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: