Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazawa waachiwa msala wa kiatu WPL

Wazawa WPL Wazawa waachiwa msala wa kiatu WPL

Sun, 19 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ni wazi msimu huu kwenye vita ya ufungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) umekuwa bora na ushindani wa aina yake hasa kwa mastraika wazawa.

Misimu miwili nyuma kiatu cha dhahabu kilibebwa na wageni, msimu wa mwaka 2022, Mrundi Asha Djafar alibeba tuzo ya mfungaji bora akiweka kambani mabao 27 na msimu uliofuata Mkenya Jentrix Shikangwa akachukua baada ya kufunga mabao 17 wote wakitokea Simba Queens.

Hadi raundi ya 15, Asha Mnunka ndiye kinara wa mabao akiwa nayo 18, akifuatiwa na Stumai Abdallah wa JKT Queens aliyetupia 16, Winifrida Gerald wa JKT aliyeweka kambani mabao nane sawa na Shikangwa, huku Asha Djafar akiwa na saba na Donisia Minja (JKT Queens) akifunga sita.

Akizungumzia juu ya kiwango bora msimu huu, Mnunka alisema malengo yao msimu huu ni kuchukua ubingwa wa ligi lakini kwa upande wake kama straika ni kuwa mfungaji bora.

“Kwangu mimi mipango yangu niliojiwekea kufunga mabao 20 lakini kama yatazidi sawa lakini malengo yangu kama mchezaji kuchukua tuzo ya mfungaji na kuisaidia timu kijumla

Kwa upande wa Stumai alisema kwake kikubwa ni kuisaidia timu yake kutimiza malengo waliojiwekea kisha suala la kiatu cha ufungaji kitafuata kama atafanikiwa kuwa mfungaji.

“Kila mtu anapambana kuhakikisha timu inafikia malengo ya kuchukua ubingwa kwangu kiatu sikipi kipaumbele sana kwa sababu hakiwezi kuisaidia timu.”

Chanzo: Mwanaspoti