Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wayne Rooney hatozaa tena

Wayne Rooney Wife Sm Wayne Rooney hatozaa tena

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tofauti na wanawake walio na mbinu tele za kuzuia mimba, wanaume hutegemea njia mbili pekee; mipira ya kondomu au kukatwa mrija wa kupitisha mbegu za uzazi (vasectomy), na ndicho alichofanya Wayne Rooney.

Mke wa mwanasoka mstaafu Wayne Rooney, Coleen, amefichua kwamba mumewe sasa hawezi tena kumtungisha mwanamke mimba kwa kuwa amefanyiwa vasectomy.

Katika mahojiano na gazeti la The Sun wiki hii, Coleen alikiri kumshawishi nyota huyo wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza, kufanya mbinu hiyo ya upangaji uzazi kwa wanaume.

“Alifanyiwa upasuaji huo baada ya mtoto wetu wa nne kuzaliwa. Nilizungumza na Rooney na akaona umuhimu wa vasectomy ili tusipate mtoto mwingine,” alitanguliza Coleen, 37.

Cass, aliye na umri wa miaka mitano, ndiye kitinda mimba wa Rooney na Coleen. Wanandoa hao wamejaliwa watoto wanne — Kai, 13, Klay, 10, Kit mwenye umri wa miaka saba na Cass.

“Kila mara nilipojifungua, wanahabari walifanya mazoea kuniuliza iwapo ningeendelea kupata watoto. Swali gumu zaidi walilotaka nijibu ni iwapo nilitamani kupata mtoto wa kike,” akasema Coleen.

“Tamanio langu lilikuwa kupata watoto wachache, kama watatu hivi. Lakini nilishawishika kutafuta binti baada ya kumzaa Kit. Nilifadhaika sana ilipotokea kuwa mtoto wetu wa nne pia ni mvulana,” .

“Nilimzungumzia Rooney kwa ukali sana na akakubali pendekezo langu la kupanga uzazi. Sikutaka mimba nyingine na akakubali kuonja makali ya kisu,” aliongeza.

Rooney, 37, alipendana na Coleen tangu wakiwa na umri wa miaka 16 kisha wakafunga ndoa mwaka 2008.

Utakumbuka Rooney amewahi kukwaruzana na mkewe mara kwa mara kuhusu michepuko na unywaji pombe kupindukia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live