Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili kuongeza nguvu Dodoma Jiji FC

Kocha Mkuu Wa Dodoma Jiji, Francis Baraza Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Francis Baraza

Tue, 2 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Francis Baraza amesema dirisha hili la usajili anatarajia kuimarisha kikosi chake kwa kufanya usajili wa wachezaji wawili kwenye eneo la ushambuliaji na ulinzi.

Baraza aliyejiunga na Dodoma Jiji kuchukua nafasi ya Kocha Melis Medo aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa mwaka jana.

Kocha Francis Baraza, amesema Ligi Kuu Tanzania Bara ni ngumu na imekuwa bora amekiona kikosi chake kinavyocheza sio timu mbaya, lakini atakachokifanya ni kuboresha kikosi kwa kuongeza wachezaji kadhaa.

“Maeneo ambayo nitaenda kuongeza nguvu ni eneo la ushambuliaji mmoja, wale nilionao hawatoshi hivyo natakiwa kuongeza mmoja ambaye atakuja kuongeza kitu kwenye kikosi cha kwanza.

“Lakini pia kwenye eneo la ulinzi natakiwa kuongeza beki mwingine kwa wale waliopo vimo vyao sio vikubwa ni wafupi, hivyo natakiwa kuangalia mlinzi mwenye kimo aje kuongeza nguvu kikosini,”amesema Baraza.

Amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara inazidi kuwa ngumu hivyo ili utimize malengo mliyojiwekea kama timu lazima muwe na kikosi bora chenye ushindani mkubwa, ndio maana ameamua kuingia sokoni kusaka nyota wawili.

Chanzo: Dar24