Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawa awatuliza presha Msimbazi

69298 Wawa+picha

Thu, 1 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI Simba kiliwasilia jana saa 1:00, usiku wakitokea Afrika Kusini ambapo waliweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kwa ndege ya Tanzania, huku beki wake kisiki, Pascal Wawa akiwatuliza mashabiki wa klabu hiyo kwamba huu ni msimu wao.

Wawa alisema anafahamu kusajiliwa kwa mabeki wengi kikosini kunaweza kuwapa mashaka ya kutojua nani watakaocheza, lakini akawaambia watulie kwani kocha ndiye mwamuzi, ila pia nyopta wote wamejipanga kuliamsha msimu huu.

"Tumefanya mazoezi ya kutosha kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi ambayo wao ndio wataamua mchezaji ambao wataanza katika kikosi cha kwanza," amesema.

"Mabeki na hata wachezaji wengine wote waliosajiliwa ni wazuri jambo ambalo litaongeza ushindani katika timu. Hata msimu uliopita kulikuwa na wachezaji wengi lakini tuliweza kucheza wote kwa pamoja na matumaini yangu hata msimu huu itakuwa hivyo, kikubwa tunawaachia makocha wao ndio watamua," alisema Wawa ambaye alisajiliwa msimu uliopita akiwa mchezaji huru.

Kabla ya kutua Msimbazi Wawa aliwahi kuichezea Azam na kuipa mafanikio makubwa ikiwamo kutwaa taji la kwanza la michuano ya Kombe la Kagame 2015 wakimaliza bila kuruhusu bao lolote akishirikiana kuunda ukuta wa chuma na Aggrey Morris.

Chanzo: mwananchi.co.tz