Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawa: Msimu ujao tutakuwa mbali

Wawa Pic Data Wawa: Msimu ujao tutakuwa mbali

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BEKI wa Simba, Pascal Wawa amesema licha ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakiishia hatua ya robo fainali anaamini msimu ujao watafika mbali zaidi.

Wawa alisema kikosi chao kimepambana kuilinda heshima ya jezi ya timu hadi dakika ya mwisho ili wafuzu nusu fainali, ingawa mwisho wa mchezo huo matokeo hayakuwa rafiki kwao.

“Mchezo haukuwa mwepesi, tulipambana muda wote, tulikosa nafasi kadhaa lakini tumejifunza. Naamini kabisa msimu ujao tutafika mbali zaidi ya sasa.”

Anasema kutokana na namna wachezaji Simba wanavyojitoa kuhakikisha wanapata matokeo ni sababu tosha msimu ujao wakifanikiwa kwenda kimataifa, watafanya maajabu zaidi ya sasa kwani watakuwa wakijiamini zaidi.

Beki huyo amekuwa na msaada mkubwa katika safu ya ulinzi akicheza sambamba na Joash Onyango, wamekuwa wakihakikisha lango la timu yao halipati kashikashi mara kwa mara na ndiyo chachu ya mafanikio ya Wekundu wa Msimbazi msimu huu akisaidiana na nyota wengine wa chama hilo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz