Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waturuki wampigia mahesabu Thiago

Thiago Alcantara Liverpool Thiago Alcantara

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo fundi wa mpira, Thiago Alcantara yupo kwenye mazungumzo ya kuachana na Liverpool na kwenda kupiga kazi huko Galatasaray ya Uturuki, imeelezwa.

Kiungo huyo wa Kihispaniola, 32, amepoteza nafasi kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Anfield, huku mkataba wake ukiwa umebakiza mwaka mmoja tu.

Na sasa Liverpool wapo tayari kumuuza kwenda Galatasaray baada ya kuona kwamba wanaweza kupata ofa nzuri.

Galatasaray ilishinda ubingwa wa ligi msimu uliopita hivyo itakuwamo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live