Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu sita mbaroni kwa mauaji ya beki wa Kaizer Chiefs

Kaizerrr Lukee Watu sita mbaroni kwa mauaji ya beki wa Kaizer Chiefs

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi wa Afrika Kusini wametangaza Jumatano hii, Aprili 10 kuwakamata washukiwa sita, wiki moja baada ya mauaji ya mwanasoka Luke Fleurs, ambaye alicheza kama beki wa kati wa klabu ya Kaizer Chiefs mjini Johannesburg.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipigwa risasi wiki iliyopita alipokuwa akijaza mafuta gari lake kwenye kituo cha mafuta katika vitongoji ya Kaskazini-Magharibi mwa jiji hilo na kutangazwa kuwa amefariki akiwa nyumbani kwake.

Washukiwa hao wamekamatwa katika kitongoji cha Soweto, kusini Magharibi mwa Johannesburg, siku mbili baada ya kugunduliwa kwa gari la Fleurs, kulingana na msemaji wa jeshi la Polisi.

Wachunguzi wanaamini washukiwa hao ni sehemu ya kundi la uhalifu linalohusika na wizi mwingine wa magari huko Gauteng, mojawapo ya majimbo tisa ya Afrika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live