Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wa gwiji wa soka Iran wazuiwa kutoka nchini

Watoto Wa Gwiji Wa Soka Iran Wazuiwa Kutoka Nchini Watoto wa gwiji wa soka Iran wazuiwa kutoka nchini

Tue, 27 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Gwiji wa soka wa Irani Ali Daei anasema ndege ya kimataifa imebadilishwa njia ili kumzuia mkewe na bintiye kuondoka nchini.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 53, ambaye ameeleza kuunga mkono maandamano dhidi ya serikali, alisema familia yake ilijaribu kusafiri kwa ndege kutoka Tehran hadi Dubai kuungana naye kwa likizo siku ya Jumatatu.

Lakini ndege hiyo ilitua kwenye kisiwa cha Irani kwenye Ghuba na wakaondolewa.

Hakuna sababu iliyotolewa na wawili hao wanarejea Tehran, Ali Daei aliongeza.

Maandamano ya hivi punde yalichochewa na kifo cha Irani-Kurd Mahsa Amini, 22, mnamo Septemba.

Alikuwa ameshikiliwa kwa madai ya kuvaa hijabu yake isivyofaa.

Zaidi ya waandamanaji 500, wakiwemo watoto 69, wameuawa, huku maelfu ya wengine wakikamatwa, wanaharakati wa haki za binadamu wanasema.

Makumi ya maafisa wa usalama wa Iran pia wanaripotiwa kuuawa.

Chanzo: Bbc