Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watford Yamtimua Claudio Ranieri

Claudio Claudio Ranieri

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Watford imemfukuza kocha wake Claudio Ranieri ndani ya miezi mitatu tokea apewe kibarua cha kuinoa klabu hiyo ambapo awali alisainishwa na kupewa mkataba wa miaka miwili.

Watford walimuajiri Ranieri mwezi Oktoba baada ya kutumikia miaka miwili nje ya Uingereza, huku kufungashiwa virago kwa Xisco Munoz, ndio mwanga mpya wa muitaliano huyo mwenye miaka 70 kupata nafasi tena ndani ya EPL.

Ranieri amefanikiwa kuingoza Watford kwenye michezo kumi na nne huku akiwa ameshinda michezo miwili tu mmoja ukiwa dhidi ya Everton kwenye dimba la Goodison Park huku mwingine dhidi ya Manchester United.

Mchezo wa mwisho aliopoteza dhidi ya Norwich City kwa 3-0 huku akiwa na hasira na wachezaji wake ambapo ukiwa mchezo wa nane kupoteza katika michezo tisa ya mwishoya ligi na vikombe, huku akiwakalipia wachezaji “kuwa yeyote mabye haelewi midumo yake anaweza kwenda nyumbani.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live