Siku tatu zimebaki kuelekea mtanange wa kukata na shoka baina ya magwiji wawili wa Soka nchini Simba dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Wakati Joto la mtanange huo likizidi kupanda kila siku zinavyosogea tayari kuna hali ya sintofahamu kuelekea mchezo huo.
Kwa mujibu wa kanuni za TFF na Ligi Kuu timu zote zinatakiwa kuvaa nembo ya wadhamini wote wawili katika jezi zao lakini simba kupitia maneno ya CEO wake wamesema hawaoni kama wanaelekea kuvaa nembo tofauti na NBC.
“Hatuwezi kuanza utekelezaji wowote mpaka tupate ufafanuzi. Hadi sasa hatujapata tumelazimishwa kupokea nembo. Kuna kikao cha maandalizi kinachosimamiwa na bodi ya ligi. Nitakwenda na mawakili kupata ufafanuzi, la sivyo hatutatekeleza maagizo hayo” Babra
Lakini kanuni zinaeleza wazi adhabu ambazo timu itakumbana nazo itakapokaidi maagizo kama hayo. Ambapo kuna faini pamoja na kushushwa daraja.