Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wamwaga wino Mashujaa FC

Mashujaa Kukwepa Kichapo Cha Sita Leo Dhidi Ya Tabora United Watatu wamwaga wino Mashujaa FC

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Klabu ya Mashujaa FC imeanza kuimarisha kikosi chake baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji watatu katika dirisha hili la usajili tangu lilipofunguliwa Desemba, mwaka jana.

Nyota ambao hadi sasa wamemwaga wino wa kuitumikia Mashujaa ni Nyenyezi Juma kutoka Inter Stars inayoshiriki Ligi Kuu ya Burundi, Balama Mapinduzi mchezaji huru baada ya kuachana na Coastal Union na Emmanuel Mtumbuka kutoka Stand United.

Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amesema kuwa lengo la kufanya usajili huo ni kuimarisha kikosi chao ambacho kiko nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

“Tunataka kutumia dirisha hili la usajili kujiimarisha, hatuko kwenye nafasi nzuri sana kwenye msimamo wa ligi, hivyo tunapaswa kubadilika na wakati ndio huu wakati Ligi Kuu ikiwa imesinmama.

“Kuna baadhi ya wachezaji tunaenda kuachana nao kwenye kipindi hiki na kuleta nyota wapya ambao watakuja kuleta kitu kipya na kutuondoa mahali tulipo hivi sasa,” amesema Baresi.

Chanzo: Dar24