Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania watoswa urefa CHAN

Chan Pic Data Watoswa Waamuzi kutoka Tanzania

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati jumla ya marefa 32 na wakufunzi wanne wakiteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) kushiriki programu za mazoezi kwa ajili ya kuchezesha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (Chan), hakuna Mtanzania aliyepata fursa ya kuwemo katika orodha hiyo.

Waamuzi wa kati 24, waamuzi wasaidizi 25, marefa wanne kwa ajili ya Teknolojia ya usaidizi wa video (VAR) pamoja na wakufunzi wanne wameteuliwa katika orodha hiyo ambayo imefungia milango Watanzania.

Marefa wanne waliochezesha mechi za hatua ya awali ya mashindano ya klabu Afrika kwa timu za Tanzania, Simba, Yanga na Azam wamefanikiwa kuingia katika orodha hiyo iliyojaza kundi kubwa la waamuzi na wakufunzi kutoka Misri.

Mahmood Ismail aliyechezesha mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi amecheguliwa kushiriki mafunzo hayo huku akiwemo pia Abongile Tom wa Afrika Kusini aliyechezesha mechi ambayo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Primeiro de Agosto ya Angola, Jumapili iliyopita.

Kuna refa Samuel Uwikunda aliyechezesha mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Yanga na Al Hilal iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wiki mbili zilizopita.

Georges Gatogato wa Burundi ambaye alishika kipyenga katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho ambayo Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Akhdar ya Libya naye amefanikiwa kuwemo katika orodha hiyo ya waamuzi walioitwa kwenye mazoezi hayo.

Marefa wa kati waliochaguliwa ni Loufti Bekouassi wa Algeria, Milazar Patrice (Mauritius), , Georghes Gatogato (Burundi), Souleiman Djama (Djibout), Allaou Mahamat (Chad), KalilouTraore (Ivory Coast), Adel Mohamed (Misri), Abdelaziz Bouh (Mauritania), Mutaz Ibrahim (Libya), Sabri Karim (Morocco), Atcho Pierre (Gabon), Gnama Akiesso (Togo) na Celso Alavacao wa Msumbiji.

Wengine ni Joseph Odey (Nigeria), Samuel Uwikunda (Rwanda), Mahmood Ismail (Sudan), Messie Mvoutou (Congo), Mehrez Melki (Tunisia), Hougnandande Louis (Benin), Daouda Gueye (Senegal), Tom Abongile (Afrika Kusini), Ali Mohamed (Niger), Ngwa Blaise (Cameroon) na Jammeh Lamin (Gambia).

Upande wa marefa wasaidizi walioteuliwa ni Abbes Zerhouni wa Algeria, Clemence Kanduku (Malawi), Jospin Malonga (Afrika ya Kati), Gamal Samir (Misri), Mathew Kanyaga (Namibia), Styven Moutsassi (Congo), tere Mamady (Guinea), Kwasi Brobbey (Ghana0, Diba Hamedine (Mauritania), Ngoh Desira (Ivory Coast), Abdul Jawo (Gambia), Hamza Abdi (Somalia), Yacouba Aziz(Niger).

Wengine ni Samake Modibo (Mali), Dos Reis Miro (Sao Tome na Principe), Ditsoga Marlaise (Gabon), Menye Rodrigue (Cameroon), Emery Niyongabo (Burundi0, Nouha Bangura (Senegal), Sanou Judical (Burkina Faso), Dieudonne Mutuyimana (Rwanda), Eric Ulrich (Benin), Ivanildo Olivira (Angola), Hensley Pretrousse (Shelisheli) na Ayman Ismail (Tunisia),

Waamuzi kwa ajili ya VAR ni Elghandour Ahmed (Misri), Issay Sy (Senegal), Pacifique Ndabimana (Burundi), Mahmoud Ashor wa Misri. wakati wakufunzi wa marefa ni Celestin Ntagungira (Rwanda), Malang Diedhiou (Senegal), Jean-Claude Birumushahu (Burundi0, Elsayed Mourad (Misri), Mohamed Gabon (Djibouti), Mohamed Khater (Misri)

Chanzo: Mwanaspoti