Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania kukipiga na Tottenham, Wolves

Tottt 024 05 14 At 14.jpeg Watanzania kukipiga na Tottenham, Wolves

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juhudi za Serikali kuitumia Michezo kama sehemu ya ajira kwa vijana zimeendelea kuungwa mkono na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo, wakiwa na lengo la kuhakikisha kilele cha mafanikio kinafikia kwa miaka ya usoni.

Serikali ya awamu wa Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikisisitiza suala la kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana katika vituo mbalimbali vya michezo, Shule za Msingi na Sekondari nchini.

Katika kuhakikisha hilo linatimizwa, Shule ya Kimataifa ya Al-Irshaad iliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam imewataka Watanzania kupeleka watoto wao kupata elimu shuleni hapo ili kuvumbua na kuendeleza vipaji vya vijana.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Salim Sadiq amesema swala la kukuza vipaji na kuviendeleza ni la kipaumbele chao kwani katika Ulimwengu wa sasa vipaji vinalipa na kuchangia pato la Taifa.

“Unaona wachezaji wakubwa mpira wa miguu, riadha hata kuogelea wanavyoingiza pesa nyingi kutokana na vipaji vyao na hivyo kuchangia pato la taifa, sasa sisi hapa ndipo mahala pake pa kusaidia vijana wenye vipaji kufikia malengo yao.

Mkuu huyo wa shule anasema shule hiyo inafundisha masomo yake kwa mtaala wa Cambridge na hivyo kuwapa vijana fursa kupata elimu bora kuanzia Shule Msingi hadi Sekondari Darasa la Tisa.

Wanafundisha pia masomo ya Dini ya Kiislam, Lugha ya Kiarabu na Quran tukufu, lengo ni kujenga taifa lenye maadili mema.

Kuhusu masomo ya ziada Mkuu huyo wa shule anasema kwamba kuna club mbalimbali za vijana kama Kuogelea, Mpira wa Miguu, Karate na fani mbalimbali za kazi za mikono mfano mapishi na kushona.

Masomo yanalenga kuwafanya vijana kijitegemea sababu yameegemea zaidi katika vitendo kuliko nadharia.

Katika hatua nyingine amesema Timu ya Mpira wa miguu iko mbioni kwenda Uingereza kucheza na washirika wao klabu maarufu za soka nchini humo za Tottenham na Wolverhampton, wana waalimu wa daraja la juu katika fani zote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live