Watu watano wanashikiliwa na vyombo vya Usalama vya Ubelgiji baada ya shabiki wa klabu ya Manchester City kushambuliwa wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Club Bruges.
Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 63, alitishiwa maisha wakati ametoka kutazama ushindi wa City wa magoli 5-1.
Shambulizi hilo limefanyika katika eneo la E40 Drongen, kilomita 45 kutoka Bruges.
Katika taarifa yake Klabiu ya Man City imesema "wameshitushwa na wamehuzunisha na tukio hilo", wakati klabu ya Bruges wamesema "wameogopeshwa na tukio hilo".
Taarifa kutoka katika vyombo vya usalama zinasema; " Mwanaume aliekuwa amevalia skafu ya Manchester City alisimamisha gari yake baada ya mchezo na kuingia katika moja ya duka lililokuwa katika maeneo hayo".
"Kutokana na uchunguzi wa awali, Skafu yake ilichukuliwa akiwa ndani ya duka na mshukiwa na kutoka nayo nje, ghafla muathirika wa tukio akaingia katika mzozo na mshukiwa katika eneo la kuegeshea magari na akaishia kudondoka chini baada ya shambulio la kimwili".
"watu wa huduma ya kwanza walifika kwenye tukio, na kumuwahisha mwathirika hospitali, na alikuwa katika hali mbaya.
Kutokana na tukio hilo Polisi inawashikilia watu watano.
Katika taarifa yake klabu ya Bruges imesema" Kwa nguvu zote tunapinga vitendo vya kihalifu, kote ndani na nje ya uwanjan, tunaweka uvumilivu mbele, wakaongeza "tuko pamoja na familia na marafiki zake"